Mabalozi wafunguka kinachowakuna kwa JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya Sherehe za Mwaka mpya kwa Mabalozi(New Diplomatic Sherry Party) Ikulu jijini Dar es Salaam. Februari 10,2017
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, wamempongeza Rais Magufuli pamoja na serikali ya awamu ya tano kwa jitihada zake za kupambana na rushwa, kujenga nidhamu kwa watumishi wa umma na kuimarisha uchumi.