Vita ya dawa za kulevya yatinga Serengeti Boys
Katika harakati za kuendelea kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, Shirikisho la Soka nchini TFF, linatarajia kuwapeleka vijana walio katika timu ya taifa ya Serengeti Boys katika kituo cha kusaidia waathirika wa dawa za kulevya cha Bagamoyo.