JPM: Serikali haitatoa chakula bure kwa wenye njaa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kuwa Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaopatwa na njaa ilihali wanaweza kuzalisha chakula katika maeneo yao.