Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kiongozi wa kimila wa kabila la Wahehe Chifu Adam Mkwawa wakati wa sherehe za Mei Mosi Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa Mei 1, 2018. (Picha kutoka Maktaba)
Serikali imesema inawatambua machifu wa mila waliopo nchini kutokana na kuchangia shughuli nyingi za kiserikali na kushirikishwa zikiwemo mbio za mwenge wa uhuru zinazofanyika kila mwaka.