
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kiongozi wa kimila wa kabila la Wahehe Chifu Adam Mkwawa wakati wa sherehe za Mei Mosi Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa Mei 1, 2018. (Picha kutoka Maktaba)
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Juliana Shonza, wakati akijibu swali la Mh. Taska Mbogo Mbunge wa viti maalum katika mkutano wa 11 kikao cha 48 wa Bunge la Jamhuri unaofanyika jijini Dodoma.
"Serikali inawatambua machifu na watemi wa makabila yote 124 na wanashirikishwa kwenye shughuli mbalimbali za kitaifa ili waweze kusaidia kurekebisha maadili kwa jamii", amesema Shonza.
Naye Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema ili kuenzi mila na utamaduni hivi karibuni alihudhuria maadhimisho ya kituo cha kumbukumbu ya utamaduni wa kabila la Wasukuma Bujora jijini Mwanza na kukutana na machifu wengi wa kabila hilo na kupewa cheo cha manju mkuu wa ngoma.