Dereva wa basi lililowaka moto asakwa
Baada ya gari la abiria linalofanya safari zake Arusha - Dar es salaam kuteketea kwa moto maeneo ya Tegeta, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma amesema bado wanamsaka dereva wa basi hilo ili kuweza kutoa maelezo ya kina juu ya ajali hiyo.