Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) David Beasley zawadi ya Picha moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini pamoja na kinyago cha mpingo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya wakulima kukosa soko la mazao ya ziada serikali ipo tayari kuruhusu chakula kuuzwa nje ya nchi.