CHADEMA yamkana Mbunge wake
Baada ya Mbunge wa Jimbo la Ukerewe mkoani Mwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Michael Mkundi kutangaza kujiuzulu na kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) usiku wa jana Oktoba 10, CHADEMA wamekanusha tuhuma alizozitoa dhidi ya chama hicho.