Mkuu wa Mkoa, TRA wageuza Machinga kuwa walinzi
Serikali ya mkoa wa Kagera imewataka wafanyabiashara wadogo 'Machinga' kuwa walinzi kwa kutoa taarifa ya wafanyabiashara ambao wameanza kupunguza bidhaa katika maduka yao kwa lengo la kupewa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo, huku ikisisitiza kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua.

