Waziri Jafo aipa Dar es salaam siku 6 tu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa muda wa siku 6 kuanzia leo Desemba 13, 2018 hadi Jumatano ijayo Desemba 19, 2018, kuhakikisha halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaanza ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis.