Kangi awasimamisha kazi maofisa watano
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasimamisha kazi maofisa 5 wa idara ya wakimbizi wakituhumiwa kutoripoti uwepo wa nguo 1,947 zinazodaiwa ni za jeshi la Burundi, kwenye kambi za Nduta na Mtendeli zilizopo Mkoani Kigoma.

