CHADEMA wamjibu Kakobe, wakumbushia kauli yake
Baada ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship nchini Tanzania, Zachary Kakobe, kuwataka viongozi wa CHADEMA waliotoa maneno machafu kwa viongozi wa dini kutubu haraka iwezekanavyo, baadhi ya viongozi wamemjibu kwamba anapaswa kupuuzwa, yeye ndiye atakayetumbukia kwenye shimo.

