Msimamo wa TZ kuhusu kauli ya Jaguar
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Kenya imekanusha kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar kuwa si kauli ya Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.