Kabendera ashtakiwa makosa ya utakatishaji fedha
Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera leo Agosti 5, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu ikiwemo utakatishaji fedha wa zaidi ya shilingi milioni 173, kukwepa kodi pamoja na njama ya kutenda kosa la jinai.