Mwijaku amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital ambapo amezungumzia ndoa ya MC Pilipili kuwa watu wamuache apate raha kwakuwa kuoa kuna raha nyingi na ikizingatiwa kuwa yeye amecheza sana na waschana wengi.
“Ndoa tamu muacheni Mc Pilipili apate raha maana amechovyachovya sana, amehangaika, ameteseka na amepambana kumpata mke wake Philomena Thadey kwahiyo muache apumzike ale maisha yake”
Aidha kuhusu wanaomponda mke wa MC Pilipili kuwa hana kazi, Mwijaku amesema kuwa yeye hawezi kumcheka wala kumdhihaki kwa sababu kupata kazi ni majaliwa ya Mungu na atapata ni suala la muda ukifika.