Amuua mwanaye kisha akajisalimisha Polisi
Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Philipina Silayo, mkazi wa Kijiji cha Kitangara Wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni mwanaye wa miaka mitano.

