"Mitaala imewekwa kwa roho mbaya"- Waziri Jafo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ameagiza wataalamu wa mitaala ya elimu hapa nchini kukaa na kutazama miongozo ya elimu iliyopo, kwani imewekwa kwa roho mbaya na inamnyima mwanafunzi uhuru wa kuchagua kusoma fani anayoipenda.

