Mahakama yakataa Erick Kabendera kumzika mama yake
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, leo Januari 2, 2020 imekataa ombi la Mwandishi wa habari Erick Kabendera, kushiriki katika ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi Verdiana Mjwahuzi aliyeaga dunia Disemba 31, 2019, yatakayofanyika Januari 3, mwaka huu, Kanisa Katoliki.

