Wanafunzi Elfu 59 waliofaulu wakosa madarasa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, amesema jumla ya wanafunzi Elfu 59,765 sawa na asilimia 7.86 ya Wavulana na Wasichana waliofaulu kwenda kidato cha kwanza, hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.