"Mkapa ameacha alama kwa kizazi cha sasa" -Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, ametuma salamu za rambirambi na kutoa pole kwa familia ya Rais Mstaafu Hayati Benjamin Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Magufuli pamoja na kwa Rais wa Zanzibar na Serikali zote mbili na chama cha CCM kwa msiba mzito kwa Taifa.

