Baada ya mke na dada kuuawa baba naye auawa
Baba wa familia na mkazi wa barabara ya nne jijini Tanga Alii Bagidad (60) mwenye asili ya Kiasia ambaye mke wake pamoja na dada wa kazi walikutwa wamenyongwa pamoja na kutobolewa macho yao wiki iliyopita na yeye amekutwa amekufa baada ya mwili wake kuokotwa katika eneo la Nguvumali B.