Gamondi bado yupo sana Yanga SC

Yanga itashuka tena dimbani baada ya lenda ya FIFA kukabiliana  na Al Hilal katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa Novemba 26 2024.Baada ya kupokea kipigo dhidi ya Tabora United kuna taarifa nyingi zilienea kwenye vijiwe vya mpira na mitando ya kijamii kuhusiana na Kocha wa timu hiyo kuwekwa kitimoto na Uongozi wa kikosi cha Wananchi.

Klabu ya Yanga imesema hakuna kikao chochote kilichoendelaea baina ya uongozi na kocha mkuu wa kikosi hiko Miguel Gamond baada ya kufungwa magoli 3-1 dhidi ya Tabora United katika uwanja wa Azam Complex Jana  Dar es Salaam.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS