Yanga itashuka tena dimbani baada ya lenda ya FIFA kukabiliana na Al Hilal katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa Novemba 26 2024.Baada ya kupokea kipigo dhidi ya Tabora United kuna taarifa nyingi zilienea kwenye vijiwe vya mpira na mitando ya kijamii kuhusiana na Kocha wa timu hiyo kuwekwa kitimoto na Uongozi wa kikosi cha Wananchi.
Klabu ya Yanga imesema hakuna kikao chochote kilichoendelaea baina ya uongozi na kocha mkuu wa kikosi hiko Miguel Gamond baada ya kufungwa magoli 3-1 dhidi ya Tabora United katika uwanja wa Azam Complex Jana Dar es Salaam
“Hakuna mtu anayepokea vizuri kufungwa na hili limetokea kwa bahati mbaya kutokana na kusimamishwa kwa baadhi ya wachezaji kwa kadi nyingi za njano na wengine kukabiliwa na majeraha ndiyo sababu ya kupoteza katika mechi ya jana na tumeyapokea matokeo basi tunajipanga kwa mechi zijazo” @alexngai85 Alex Ngai Mjumbe wa kamati tendaji Yanga SC
Yanga itashuka tena dimbani baada ya lenda ya FIFA kukabiliana na Al Hilal katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa Novemba 26 2024.Baada ya kupokea kipigo dhidi ya Tabora United kuna taarifa nyingi zilienea kwenye vijiwe vya mpira na mitando ya kijamii kuhusiana na Kocha wa timu hiyo kuwekwa kitimoto na Uongozi wa kikosi cha Wananchi.
Swali gumu ambalo wangekutana nalo Viongozi wa Yanga SC kama kweli wangemfukuza Gamondi lingekuwa sababu ya kwa nini Mkufunzi huyo anafukuzwa? kufungwa mechi mbili iwe sababu ya kumfukuza Kocha? Timu hiyo bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara ianshika nafasi ya pili tena kwa tofauti moja baina yao na Watani wao wa jadi Simba SC hiyo iwe sababu ya kumtimua kazi Mwalimu?
Gamondi raia wa Argentina amejiunga na Yanga SC msimu wa 2023-2024 kuchukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyetimkia nchini Morocco kufundisha kikosi cha FAR Rabat ambaye aliifikisha timu hiyo kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Uongozi wa Yanga umethibitisha Muargentina huyo bado yupoyupo sana kwa Wanachi kwasasa wanajipanga na michezo ijayo ya ligi kuu na michuano ya klabu bingwa Afrika. Wachezaji wengi wa Wanajangwani hawachezi kwenye viwango vyao vilivyozoeleka hiyo inatajwa kuwa moja ya sababu ya kuyumba kwao msimu huu.Mshambuliaji aliyetabiriwa makubwa kabla ya kujiunga na mabingwa wa kihistoria ligi kuu Tanzania Prince Dube raia wa Zimbabwe hajaanza vizuri maisha yake mapya kwa Waajiri wake wapya baada ya kauchana na Azam FC.
Miguel Gamondi anakazi ya kuhakikisha anarudisha viwango vya nyota wake kabla ya kurejea kwa ligi kuu na michezo ya klabu bingwa Afrika. Kazi ya kutetea ubingwa itakuwa ngumu kutokana na ugumu unaoendelea kwenye ligi na kama Yanga SC inahitaji kufanya vizuri msimu huu na kutetea ubingwa wake pamoja na kufanya vizuri mashindano ya kimataifa wanapaswa kumbakisha mtaalamu huyo kikosini.
Hakuna timu isiyofungika Duniani itakuwa kwenye ubora mkubwa ila kuna muda itashuka kwa sababu mbalimbali hivyo inapaswa kupata muda wa kuangalia mapungufu yake kisha kuyanyia kazi ili kurudisha makali yake ya zamani.