Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya shirikisho la Soka nchini TFF Tangu kujiunga na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni FIFA Mwenyekiti Kamati ya Bunge na Maendeleao ya Jamii, Said Mtanda amesema, hapo zamani wachezaji walikuwa hawana maslahi kama hivi sasa ambapo soka linatumika kama biashara.
Mtanda amesema, endapo serikali itawekeza juhudi na nguvu kubwa katika kuandaa mazingira mazuri ili vijana waweze kujiajiri kupitia soka, nchi itaweza kuinua uchumi na kutakuwa na uwezo wa kutengeneza ajira nyingi na kukabiliana na changamoto ya tatizo la ajira kwani serikali haina uwezo wa kuajiri vijana mbalimbali wenye vipaji lakini sekta binafsi.
Mtanda amesema, wagombea mbalimbali wanaotangaza nia wamekuwa wakiahidi kuinua soka hapa nchini bila kuweka mikakati madhubuti na yakisasa ya kuona namna watakavyowekeza kwenye mpira wa miguu ili kuleta tija tunayoitegemea.
hafla hiyo imeambatana na zoezi la uzinduzi wa jezi mpya za Timu ya Taifa taifa Stars pamoja na ugawaji wa vyeti kwa waliochangia ukuaji wa soka nchini,