Sunday , 24th May , 2015

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi la Super Feo lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Songea kutumbukia Mtoni eneo la Tazama Pipeline Inyara.

Basi LA Super Feo linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Songea likiwa limetumbukia mtoni Leo asubuhi.

Akizungumza na East Africa Radio Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Nyigesa Wankyo amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya basi hilo namba T481BNT kutumbukia katika mto Shamongo eneo hilo la Inyara.

Kamanda Wankoyo amesema kuwa kati ya watu watatu waliofariki dunia ni raia wawili wa Tanzania na mmoja ni Marekani ambae alitambuliwa na wenzake waliokuwa wanasafiri nae.

Aidha ameongeza kuwa watu karibu wote waliokuwa kwenye gari hiyo ambao wanakadiriwa nia 45 wamejeruhiwa kutokana na ajali hiyo na kusema kuwa bado walikuwa katika eneo la tukio ili kulitoa gari hilo na kujua ni amdhara gani zaidi yamepatika.