Thursday , 14th May , 2015

Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO, linakusudia kupanga viwango vipya vya malipo ya umeme vitakavyotoa unafuu kwa taasisi hiyo na wadau wake endapo vyombo vinavyohusika ikiwamo EWURA vitaidhinisha.

Jengo la Shirika la Umeme nchini Tanzania TANESCO mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mipango Mikakati kutoka Tanesco Makao Makuu, Patrick Sankara katika mkutano ulioandaliwa na TANESCO, kilichofanyika jana mkoani DODOMA kwa lengo la kupata maoni kutoka kwa watumiaji.

Amesema TANESCO ina mpango wa kuanza kugawa viwango hivyo vipya kulingana na matumizi na wale watakaobadili muda wa matumizi watapatiwa punguzo maalumu kwenye viwango vyao vya malipo ya umeme.

Amesema matumizi ya umeme kwa sasa hupanda ghafla kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku na kusababisha msukumo wa umeme kutoka katika vyanzo vyake kupunguza na kusababisha TANESCO kuwasha mashine za ziada kufidia mzigo.