
msanii wa miondoko ya dance hall nchini Uganda marehemu Vicent Semmambo aka 'Moroz'
Kifo cha Moroz kinakuja ikiwa ni siku chache tuu baada ya msanii Harriet Kisakye kufariki na ikiwa ni kipindi kisichozidi pia miezi miwili tokea nyota mwingine Kinda katika tasnia hiyo, kuaga dunia pia.
Salamu za rambirambi zimeendelea kumiminika kutoka kwa wasanii na wadau na mashabiki wa muziki nchini Uganda kufuatia kifo cha msanii huyo ambapo taarifa zaidi kuhusiana na maziko yake zitatolewa hivi karibuni.
Moroz alikuwa ni moja ya wasanii wanaochipukia wa miondoko ya dancehall ambaye hivi karibuni aliachia video yake mpya inayoitwa 'Amasala' na alishirikiana pia na msanii GNL Zamba.
