Tuesday , 21st Apr , 2015

Baraza la Michezo nchini BMT limesema linatarajia kuongeza muda wa kuchukua fomu za wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Chama cha Bardmintony (Vinyoya) nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa BMT, Najaha Bakari amesema, mpaka sasa wagombea waliochukua fomu ni saba ambapo wanaamini wakiongeza muda kwa ajili ya wagombea hao kuchukua fomu itasaidia kuweza kupata wagombea wengi na wenye sifa watakaoweza kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi huo.

Najaha amesema, uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Aprili 25 mwaka huu ambapo kama muda ukiongezwa pia wanatarajia kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi huo ambapo mwisho wa kuchukua fomu kwa wagombea ulikuwa ni April 15.