Friday , 17th Apr , 2015

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa amewaomba wakazi wa manispaa ya Dodoma kushirikiana naye katika kutimiza ujenzi wa maabara za shule za sekondari zilizoko katika manispaa hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi. Betty Mkwasa

Mkwasa ameyasema hayo leo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali wa mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwaomba wamsaidie katika ujenzi huo wa maabara.

Amesema tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma miezi miwili iliyopita amekuta ujenzi wa maabara ukisuasua na kwamba hali ni mbaya kwani mpaka sasa wamejenga maabara hizo kwa asilimia 12 tu.

Kwa upande wake, afisa elimu sekondari, Manispaa ya Dodoma Rehema Urio alisema suala la ujenzi wa maabara ni la kila mwananchi ambapo amewaomba wananchi kuonesha ushirikiano mkubwa katika kutekeleza suala hilo.