Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kuisambaratisha Iran ikiwa haitakubali makubaliano ya kukomesha vita.
Hayo yameelezwa Jumatano usiku na Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa viongozi waliosalia wa utawala wa Iran wana fursa nyingine ya kushirikiana na Rais Trump, kuachana kabisa na mipango yao ya nyuklia na kuacha kuitishia Marekani na washirika wake.
Leavitt amesema kuwa rais Trump anatoa kipaumbele kwa amani na hakuna haja ya kuwa na vifo na uharibifu zaidi huku akiionya Iran.
Tehran imesema inalipitia pendekezo hilo lakini haina nia ya kujadiliana.
Licha ya baadhi ya maafisa wa Iran kutaja kuwa nchi hiyo ilipokea pendekezo la Marekani wa kuvimaliza vita vya Mashariki ya Kati . Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema Tehran haina nia hiyo.



