Thursday , 5th Mar , 2026

Peter wa P Square 'Mr P' anasema ndoto zake ilikuwa kucheza soka la kulipwa barani Ulaya lakini hatima yake ikaangukia kwenye muziki ambao umemtambulisha vizuri.

Picha ya msanii Mr P

Kupitia post yake mpya Mr P ameeleza kuhusu ndoto zake za mpira na muziki akiandika 

"Kamwe usikate tamaa, nilikuwa nacheza mpira na kufanya muziki pamoja, nilipewa nafasi ya kuichezea Plateau United lakini ndoto yangu ilikuwa kucheza mpira Ulaya"

"Kwa namna fulani hatima iliichagua Mic badala ya mpira, leo hii mimi ni mwanamuziki mahiri na mwenye mafanikio. Hicho si kingine ila neema" Peter P Square