Thursday , 26th Mar , 2015

Chama cha wananchi CUF kimesema kura ya maoni ya katiba mpya haitakuwepo kutokana na mwenendo wa mchakato wa zoezi la uandikishaji upya wapiga kura kupitia mfumo wa BVR kukumbwa na kasoro na kutokumalizika kwa wakati.

Abdul Kambaya

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF Bw Abdul Kambaya amesema tume ya uchaguzi imeshindwa kufikia lengo la kukamilisha zoezi la uandikishaji kama ilivyopangwa na kwamba haiwezekani kukamilisha kabla ya tarehe ya upigaji kura iliyopangwa hivyo kutaka tume kuendelea na zoezi hilo kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu na sio suala la maoni ya katiba.

Aidha Kambaya amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa maamuzi ambayo yatasaidia wananchi kupata haki ya kikatiba kupiga kura na kutoa maoni kwa wakati mwingine na kuzitaka mamlaka husika kuheshimu maamuzi yaliyofanywa na viongozi wa dini nchini kuhusu kuahirishwa kwa zoezi la upigaji kura kwani wao ndio wenye kusimamia idadi kubwa ya wananchi.