Wednesday , 28th Jan , 2026

Wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mheshimiwa Fadhili Liwaka, ametoa mfano kutoka katika kitabu kitakatifu cha Biblia,

..akielezea safari ya Wana wa Israel kutoka kwa Nabii Musa hadi Nabii Yoshua, na kuifananisha na safari ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maelezo yake, Mheshimiwa Liwaka alinukuu Yoshua 1:6 isemayo: “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.”

Alisema nukuu hiyo inabeba ujumbe wa ujasiri, uvumilivu na dhamana ya uongozi, akieleza kuwa kama ilivyokuwa kwa Yoshua, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amechukua jukumu la kuongoza taifa katika kipindi chenye changamoto, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na imani katika kufanikisha safari ya maendeleo ya nchi.