Wednesday , 17th Dec , 2025

Mashuhuda wameeleza kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia December 17, 2025 kufuatia mvua iliyoambatana na upepo pamoja na ngurumo za radi

Mvua iliyoambatana na upepo imeezua paa la nyumba katika mtaa wa Ligula TES Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.

Mashuhuda wameeleza kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia December 17, 2025 kufuatia mvua iliyoambatana na upepo pamoja na ngurumo za radi.

Aidha, wamesema kuwa hakuna athari zozote za kibinadamu zaidi ya nyumba kuezuliwa na baadhi ya mali kuharibiwa kwa maji yaliyotokana na mvua hiyo.