Friday , 28th Nov , 2025

“Novemba 26, 2025 asubuh“Novemba 26, 2025 asubuhi raia wema wa mtaa wa Riverside, kata ya Mwembesongo walitoa taarifa kuhusu mashai raia wema wa mtaa wa Riverside, kata ya Mwembesongo walitoa taarifa kuhusu mashaka na kutoonekana kwa mtoto ambaye alizaliwa kwa umri wa miezi saba ya mimba,”

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia Pendo John Matongo (19) na Kumbuka Kwalitaho (22), wakulima na wakazi wa Mwembesongo kwa tuhuma za mauaji yam toto mchanga aitwaye Selina Kumbuka (wiki 3).

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama iliyotolewa jana Novemba 27,2025 imesema kuwa tukio hilo limebainika juzi, 25 Novemba majira ya asubuhi katika eneo la mtaa wa Mchuma, Kata ya Kichangani, manispaa ya Morogoro ambapo maiti ya huyo ilikutwa ikiwa imetupwa na kutelekezwa na wawili hao.

“Novemba 26, 2025 asubuhi raia wema wa mtaa wa Riverside, kata ya Mwembesongo walitoa taarifa kuhusu mashaka na kutoonekana kwa mtoto ambaye alizaliwa kwa umri wa miezi saba ya mimba,” Kamanda Mkama alisema na kuongeza kuwa kutokana na taarifa hizo watuhumiwa walikamatwa na kusaidia kuonyesha sehemu walipotupa mwili huo baada ya kuua kwa kuziba mfumo wa hewa.

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia ambapo mwanaume aliamini kuwa si mwananye na kutoa sharti la kuuawa ili mapenzi yao yaendelee.

Jeshi la polisi limewashukuru wananchi wema walioshiriki katika kutoa taarifa zilizosaidia kubainika kwa tukio hilo.