Wednesday , 22nd Oct , 2025

Akizungumza na EATV kuhusu suala la wapiga kura waliopoteza kadi za kupigia kura, Anamary amesema wanaweza kutumia pasi zao za kusafiria, au leseni ya udereva.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Uyole ya Mbeya Mjini Mkoani Mbeya Anamary Joseph anasema maandalizi yamekamilika kuelekea uchaguzi mkuu hivyo wananchi wajitokeze siku ya Oktoba 29 kuchagua viongozi wanaowataka.

Akizungumza na EATV kuhusu suala la wapiga kura waliopoteza kadi za kupigia kura, Anamary amesema wanaweza kutumia pasi zao za kusafiria, au leseni ya udereva.

Haya yanajiri wakati joto la uchaguzi mkuu wa Rais Ubunge na Udiwani nchini likiendelea kupanda huku wananchi na wakazi wa Mbeya wajkisema kuwa wapo tayari kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanawataka ili wawaongoza katika kipindi cha miaka mitano.