.jpeg?itok=89V4E8H-×tamp=1760681795)
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu Hamisi Jamali Mkufya (22) na Abdallah Sebo (20), wakazi wa Mbugani, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Mikanjuni, Wilaya ya Tanga.
Tukio hilo lilitokea mnamo 26 Desemba 2023 katika eneo la Mikanjuni, Wilaya ya Tanga. Baada ya tukio, taarifa ziliporipotiwa Kituo cha Polisi Tanga, watuhumiwa walikamatwa na upelelezi kuanza mara moja.
Mnamo 27 Desemba 2023, watuhumiwa walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Tanga kujibu kesi ya jinai, kabla ya jalada hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga chini ya kesi namba CC No. 27880/2024, mbele ya Mheshimiwa Jaji Kobelo, ambapo walikana mashitaka yao.
Baada ya ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kusikilizwa, mnamo 16 Oktoba 2025, Mahakama iliwakuta watuhumiwa wote na hatia na kuwahukumu kifungo cha maisha jela.