
- Ikiwa kama ni kweli tunasikiliza mazungumzo yako basi tutakuwa tunakiuka haki ya faragha kwa watumiaji wetu
- Betri ya simu yako ingekuwa inaisha kwa haraka kwa sababu microphone ingekuwa inafanya kazi muda wote.
Na kama huamini kwenye haya mawili Adam anaongeza ufafanuzi kwa kusema:
- Ukiona Tangazo umeliona kwenye timeline yako basi fahamu fika ni moja ya kitu ambacho umekuwa ukikitafuta kwa ukaribu kwenye mtandao huo.
- Instagram hushirikiana na watangazaji (advertisers) wanaolipia kufikia watu wenye Kundi au uhitaji wa kitu fulani, na siyo kwa kusikiliza mazungumzo binafsi.
Kwa kifupi: Instagram haikusikilizi, bali inakuonyesha kile unachokihitaji mtandaoni.