Monday , 4th Aug , 2025

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha McMaster nchini Canada umebaini kuwa kusikiliza wanawake kunaleta maamuzi bora zaidi. Wanawake wakishirikishwa kwenye nafasi za juu, kampuni huimarika, makosa hupungua, na ushirikiano huongezeka.

Tafiti nyingine pia zinaunga mkono hili mfano ripoti ya Credit Suisse (2014) na McKinsey & Company zinasema makampuni yenye wanawake wengi kwenye bodi hufanya vizuri zaidi kibiashara.

Hitimisho:
Ni muda wa wanawake kutopewa nafasi kwa huruma, bali kwa sababu michango yao ni ya dhahabu katika maamuzi.