Tuesday , 29th Jul , 2025

Mhusika wa mauaji ya mtanzania Dunia Tuhenya bado hajakamatwa.

Mhusika wa mauaji ya  mtanzania Dunia Tuhenya bado hajakamatwa. Mtanzania Dunia Tuhenya, 17 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la Newburgh, New York nchini Marekani.

Polisi walisema tukio hilo la kusikitisha limetokea Ijumaa usiku, tarehe 25 Julai, 2025 katika eneo la Chateau Village, kusini mwa jiji la Newburgh.

Majeraha makubwa y risasi yalipelekea kifo cha Dunia, ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya Newburgh Free Academy na nahodha wa wa timu ya soka ya eneo hilo ambaye alihamia nchini Marekani na wazazi wake mwaka 2016.