
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC ) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele amewataka waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia yale waliyojifunza kuhusu sheria mpya za uchaguzi, hasa kwa wale walioomba kupiga kura moja ya Rais katika maeneo ya magereza na kuzingatiwa kwa mchakato kwa maeneo yaliyobainishwa kuwa na mgombea mmoja .
Hayo ameyasema leo wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wasimamizi na wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo pamoja na maafisa ununuzi kutoka mikoa miwili Shinyanga na Simiyu mwenyekiti wa uchaguzi jaji wa mahakama ya rufaa Jacobs Mwambegele.
Jaji Mwambegele amesema kupiga kura ya Rais nje ya kituo kwa waliojiandikisha na namna ya kusimamia uchaguzi kwenye maeneo yenye mgombea mmoja na Magerezani ni moja ya mambo machache ambayo hayakuwepo kwenye sheria zilizopita na hakuna mwenye uzoefu nayo.
"Leo mmehitimu mkiwa na kazi kubwa mbili mnazopaswa kuzitekeleza namba moja ni kutoa mafunzo kwa wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Uchaguzi ngazi ya kata na mtayaratibu vizuri kwa weledi na mbili mtayatafsiri mafunzo kwenye usimamizi wenu"amesema Jaji Mwambegele.
Jaji Mwambegele alisema wahakikishe pia shughuli za masuala ya uchaguzi kuanzia vikao na vyama vya siasa ,utoaji fomu za uteuzi na wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani unafanyika kwa mujibu wa sheria.