Wednesday , 9th Jul , 2025

China imezindua ligi yake ya kwanza ya soka ya roboti wa humanoid huko Beijing, ikihusisha timu nne za vyuo vikuu na roboti waliotengenezwa na Booster Robotics.

Hizi roboti ni ndogo kama watoto, zinaendeshwa na AI, na zinacheza bila msaada wa binadamu zinatambua mpira, magoli, na wachezaji wenzao, na zinaweza kujinyanyua zikianguka (ingawa zingine bado zinahitaji kubebwa kwenye machela).

Mwanzilishi wa Booster Robotics, Cheng Hao, anaamini michezo kama hii itasukuma teknolojia ya roboti mbele zaidi, akilenga siku moja roboti kucheza na kushindana na binadamu. Kutakuwa na mashindano makubwa zaidi ya World Humanoid Robot Games mwezi ujao Beijing, ambapo roboti watashindana kwenye soka na michezo mingine.

Wewe ungependa kuangalia Robot World Cup?