Tuesday , 8th Jul , 2025

Mwanamuziki Ben Pol anatuambia ikitokea anaacha muziki hakutakuwa na matangazao au waraka wa kuelezea bali watu watashtukia haimbi tena na ukimya utatawala.

Katika chapisho lake la hivi karibuni kwenye mtandao wa Instagram, Ben Pol aliandika ujumbe ambao umeibua hisia mseto kwa mashabiki na wadau wa muziki. Ingawa alisisitiza kuwa hana mpango wowote wa kuacha muziki kwa sasa, alieleza wazi kuwa kama siku hiyo ikifika, hatatoa taarifa yoyote rasmi, bali watu watahisi tu ukimya wake.

 

Nukuu Kamili kutoka kwa Ben Pol:"Japo sijafikiria na sina mpango huo kabisa! lakini ikitokea siku nikaamua kuacha kufanya Muziki hakutakuwa na tangazo, wala waraka kama ambavyo miaka kadhaa nyuma watu walishtukia tu kuna mtu anaitwa Ben Pol anaimba, vivyo hivyo watashtukia kuna mtu alikuwa anaitwa Ben Pol ila siku hizi haimbi."

 

Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha hofu ya kumkosa msanii huyo ambaye ametoa nyimbo nyingi zilizogusa maisha ya watu, huku wengine wakimpongeza kwa namna alivyo na mtazamo wa kipekee kuhusu safari ya muziki.