NIC iliifunga timu ya Prisons ya Uganda kwa magoli 35-32 katika viwanja vya Gymkhana ambapo NIC inaongoza kundi A ikiwa na pointi 8, huku ikiweka rekodi ya kutopoteza mechi.
MOICT ya Kenya inaongoza kundi B ikifuatiwa na KCCA ya Kenya, ambayo iliifunga Uhamiaji kwa mabao 52-38.
Michuano hiyo inashirikisha timu za Zanzibar, Kenya, Uganda na Tanzania Bara ambapo Mashindano yaliyopita yalifanyika jijini Dar es Salaam na timu ya NIC ya Uganda iliwafunga JKT Mbweni ya Tanzania Bara katika fainali na kuchukua ubingwa kwa upande wa wanawake.