Wednesday , 2nd Jul , 2025

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, TID (Top in Dar) ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kuandika ujumbe mzito akielezea hali ngumu wanayokumbana nayo wasanii nchini, hususani kuhusu mikopo na malipo ya mirabaha.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, TID ameandika................"Mikopo Tumepigwa Chini Sawa...Basi hata hiyo Mirabaha haki yetu nayo hatulipwi na Tunajua Kuna Zaidi ya 1 Bilioni sijui hapo tunakosea wapi sisi Wajenga Nchi wenye Vipaji''

Kauli hii imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki, huku wengi wakionesha kusikitishwa na namna wasanii wanavyokosa msaada wa kifedha pamoja na kutolipwa haki zao stahiki licha ya mchango mkubwa katika sekta ya burudani.

 

TID, ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, anafahamika kwa nyimbo zilizotikisa kama "Siamini," "Zeze," na "Kiuno," na amekuwa akipaza sauti mara kadhaa kutetea maslahi ya wasanii.

 

Kwa sasa, bado haijajulikana kama mamlaka husika kama COSOTA au taasisi nyingine zinazohusika na usambazaji wa mirabaha zitatoa majibu rasmi kuhusiana na madai haya.