Monday , 30th Jun , 2025

Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80 amewataka wananchi wa Uganda kumuongeza miaka mitano mingine tena ili afanikishe lengo lake kukuza nchi hadi uchumi wa dola bilioni 500 

Rais huyo ametangaza kuwa atagombea tena katika uchaguzi mkuu ujao licha ya wakosoaji katika nchi hiyo kuonesha kukosoa baadhi ya maamuzi ya serikali yake

Museveni ameitawala Uganda tangu 1986 alipochukua madaraka baada ya kuongoza vita vya msituni na katiba imebadilishwa mara mbili wakati wa urais wake ili kumruhusu kuongeza muda wa utawala wake.

Kiongozi wa Upinzani wa Uganda Bobi Wine pia ametangaza azma yake ya kugombea urais kwa mara ya pili.