
Pichani Mbosso na Enock Bella
Katika post ambayo Bella akiomba msamaha Mbosso ameshuka na kuandika......"Kipindi Wenzetu Wawili Wametangulia Kupata Management na Kuachia Kazi Zao na Wakiwa Wanafanya Shows zao .. Mimi na Wewe Ndo Tulikuwa Tunaongea Muda Mwingi ndani pale Maskani Tabata Savanna…Niliacha Mziki na Sikuwa Nataka Mziki Kabisa Baada ya Kuona Ya Moto Band imevunjika'' Amesema Mbosso
''ila Siku niliokukuta Unalia Chumbani Peke Yako na Ukasema ‘ Nakunukuu “.. Mbosso Fanya Mziki Wewe Utanisiadia Naujua Moyo Wako ..” Nilikusikiliza na niliamua Kuanza Tena Mishe mishe Za Miziki na kwa Baraka Za Mungu Neema zilianza na nilichagua kushare na wewe Kwenye Kidogo na Kikubwa nilichopata ..,
Nilifanya Hivyo Kaka Kuanzia Kwenye Shows zangu Hadi Kwenye Maisha Ya Kawaida Kwa Ujumla … Unajua Kwa Nini …? Kwa Sababu Kauli Yako Moja ilitosha Sana Kunipa ujasiri na Leo Nipo Hapa'' Amesema Mbosso
Ujumbe huu wa Mbosso umekuja masaa machache tu baada ya Enock Bella kumuomba msamaha mwenzie Mbosso katika ukurasa wake wa Instagram mapema siku ya leo.
Bella na Mbosso wamekuwa marafiki wa muda mrefu kabla ya kujiunga na kundi lao la zamani yamoto Band na hata baada ya kundi hilo kuvunjika