Friday , 20th Jun , 2025

Katika mahojiano maalum kupitia kipindi cha SupaBreakfast kwenye segment ya #TheInterview, Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel ameipongeza EastAfricaTV na EastAfricaRadio

kwa kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa ajili ya kuzungumza moja kwa moja na Mahakama.

Prof. Gabriel amesema hatua hiyo ni ishara ya ujasiri wa vyombo vya habari vinavyoweka mbele maslahi ya taifa kwa kuchochea mijadala ya kitaifa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna Mahakama inavyotekeleza majukumu yake.

Aidha, ametoa rai kwa vyombo vingine vya habari kuiga mfano huo ili kuendelea kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu taasisi muhimu za nchi.

Tazama mahojiano haya kamili kupitia YouTube channel ya EastAfricaRadio.