
John Heche Makamu Mwenyekiti CHADEMA akihutubia wananchi wa Serengeti siku ya jana Mei 13 ambapo chama hiko kinaendele na operesheni ya No Reform No Election wakipinga uchaguzi mkuu kabla ya kufanyika mabadiliko ameweka wazi kuwa aliwahi kumshauri hayati Rais Magufuli kujenga kiwanda cha chuma ili kuepusha kuagiza chuma nje ya nchi na kufanya mzunguko wa pesa ndani ya nchi
"Wakati bwawa la mwalimu Nyerere linajengwa nikaishauri serikali chini ya Rais Magufuli, unataka kujenga bwawa unataka kujenga SGR unahitaji chuma, sisi tuna chuma pale Liganga, Ludewa tuna chuma cha kuchimba miaka 100 tuna mlima wa chuma tutatumia hiko chuma hata miaka 100, Mungu akaweka na makaa ya mawe ya kuyeyushia hiko chuma pale pale Liganga, mchanga wa kusafishia hiko chuma akaweka pale Iringa hakuna kitu tunaagiza kutoka nje"
"Nikamwambia Rais kabla hatujaanza kujenga bwawa letu la Mwalimu Nyerere tujenge kwanza kiwanda chetu kile kiwanda ambacho kilikuwa kinahitaji Dola za kimarekani Bilioni 3 ambazo ni Trilioni 7.8 halafu tuchimbe miaka 100, halafu ukishajenga hiko kiwanda kingeajiri vijana elfu 60 halafu unamuita mkandarasi ajenge bwawa la Mwalimu Nyerere unampa hela lakini unamwambia chuma utanunua hapa kwahiyo unampa hela kwa mkono huu halafu unachukua kwa mkono mwingine."
"Hawakunisikiliza wakanipuuza leo tunaagiza chuma kutoka nje, mwaka jana pekee yake tumeagiza chuma chenye thamani ya dola Bilioni 1.2 sawa na Tsh. Trilioni 3 kwa mwaka, huo ni mwaka mmoja, mwaka juizi hivo hivo kwa miaka 3 tumeagiza chuma cha Trilioni 10 ambacho tungejenga kiwanda chetu cha Trilioni 7.8 tungechimba miaka 100"