
"Moja kati ya misingi mikuu ya chama chetu ni umoja, upendo na mshikamano na kwa muda mrefu, mambo haya yamekuwa silaha tuanazojivunia ndani ya CHADEMA na yamekuwa msingi wa kusukuma dira yetu ya kupigania demokrasia ya kweli na maendeleo endelevu ya watanzania wote, na hiyo ndo sababu ya kukua chama chetu na kujijengea heshima kubwa ndani na hata nje ya nchi"
"Aidha ndani ya CHADEMA chama chetu kwa sasa chuki ya wenyewe kwa wenyewe, Chuki za sisi kwa sisi zimekuwa kubwa kuliko chuki dhidi ya mifumo kandamizi na ya kinyonyaji na pengine hata dhidi ya washindani wetu wa kisiasa ambao ni chama cha mapinduzi, vita ya ndani inmekuwa kubwa kuliko vita ya nje, nyinyi ni mashahidi maana hayo si siri tena yanafanyika hadharani kabisa na wananchi wanaona na wanatushangaa"
"Kwa kutafakari kwa kina na kwa kuunga mkono wenzetu waliokuwa viongozi kitaifa.. nimeamua kujivua uanachama wa chama hichi kama nilivyosema nimejivua si kwa kupenda"
Edward Kinabo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho leo Ijumaa Mei 9, 2025 jijini Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kutoka Temeke, Eliha Gregory, Katibu wa Bawacha Ilala, Rechael Kitamkadala, Mjumbe mkutano Mkuu Taifa, Grace Ngola na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia Bawacha, Salma Sharif.